FRANSALIAN HEKIMA SECONDARY SCHOOL
(Hosteli kwa wavulana na wasichana)
P.O. BOX-126, USA RIVER, TANZANIA
Mob.No.0789 449 947, 0756 882 711
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
YAH: MWALIKO KWA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021
WAMISIONARI WA MTAKATIFU FRANSISKO WA SALE
Jumuiya ya wamisionari wa Mt.Fransisko wa Sale ilianzishwa na Padre Petro Maria Mermier mwaka 1838 katika Nchi ya Ufaransa. Malengo yao makuu yalikuwa ni kuweka msukumo katika kazi ya kueneza Injili na kazi za misioni. Wamisionari wa Mt.Fransisko wa Sale wanajihusisha katika shughuli za kikanisa, Elimu, Elimu ya Ufundi na shughuli za kijamii kama vile miradi ya maji, kuwatunza watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kuwawezesha akinamama na kutoa huduma za kiafya.
Shirika hilo lina kanda(province) kumi na senta ya missioni tano zinazojitegemea. Kati ya kanda(province) hizi saba zipo nchini India. Mapadre wa shirika la Mtakatifu Fransisko wa Sale wanatoa huduma zao katika maeneo yafuatayo Nchi za Ulaya, America, Africa, Australia na Asia. Mwaka 1988 ndipo huduma hizo za wamisionari wa Fransisko wa Sale zilianziswa hapa Africa. Misioni ya mapadri wa shirika hilo ilipandishwa kuwa kanda ya Africa Mashariki Januari 1996. Katika bara la Africa wakati huu wamisionari wa Mt. Fransisko wa Sale wanahudumia katika nchi zifuatazo Tanzania, Kenya, Uganda, Africa ya kusini, Namibia, Swaziland, Chad, Kamerooni, Msumbiji na Zambia.
Tunaendesha shule za chekechea na shule za msingi Kigurunyembe (Morogoro), Mkuza (Kibaha/Pwani), Kagongwa na Isaka (Kahama), Ipuli, Bukene (Tabora) na shule za Sekondari Kihonda (Morogoro) na Ipuli (Tabora). Wamisionari wa Mt. Fransisko wa Sale wanaendesha kituo cha Lumen Christi, kituo cha fransalian kinachofundisha-Falsafa na maendeleo ya jamii, katika eneo la Maji ya Chai, Jimbo kuu la Arusha. Wamisionari wa Fransisko wa Sale wanaendesha shule na misioni katika nchi za Kenya na Uganda pia.
SHULE YA FRANSALIAN HEKIMA SECONDARY SCHOOL: Shule hii ya Sekondari ipo eneo la MAJI YA CHAI (Kitefu, Dolly Estate), kwenye barabara ya Arusha-Moshi.